CPA. Makalla asema Dkt. Samia amekuza utalii kaskazini kupitia ‘The Royal Tour’

Chama cha Mapinduzi (CCM) kupitia kwa Katibu wake wa NEC, Itikadi, Uenezi pamoja na Mafunzo CPA. Amos Makalla, kimeweka wazi kwamba Rais Dkt Samia Suluhu Hassan amefanya kazi kubwa katika Kufungua Milango ya Utalii kwenye Mikoa ya Kaskazini kupitia Filamu Maarufu ya ‘The Royal Tour’.

Kimesema Kupitia Filamu hiyo Maarufu iliyouteka Ulimwengu pia imesaidia kufungua Fursa Mbalimbali za Kiuchumi kwa Wananchi wa Mikoa hiyo ambapo pia pato la Serikali kupitia Utalii limeongezeka Maradufu.

CPA. Makalla ametoa kauli hiyo leo mei 04, 2025 akizungumza na Wananchi wa Babati mkoani Manyara ikiwa Siku ya Kwanza ya Ziara yake kwenye Mikoa ya Kaskazini.

“Kikubwa kilichofanyika katika mikoa ya kaskazini ni kukuza utalii kupitia ‘The Royal tour’ imefanya kazi kubwa katika mikoa ya Manyara, Arusha, Kilimanjaro kwani mapato ya utalii yameongezeka na nyie Manyara mnafaidika nao kwani mpo karibu na Karatu, Tarangire na Mbuga ya Manyara” amesema CPA. Makalla.