MKUU wa Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha Festo Kiswaga ametangaza nia ya kugombea nafasi ya ubunge katika Jimbo la Isimani lililopo mkoa wa Iringa katika Uchaguzi Mkuu wa 2025.
Kiswaga ametangaza nia hiyo mapema leo hii Juni 3, 2025 wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini Iringa huku akisema ameamua kuwania nafasi hiyo baada ya Mbunge wa sasa, William Lukuvi kutangaza mwaka 2020 kuwa hatagombea tena.
Jimbo hilo la Isimani limekuwa likiongozwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu William Lukuvi kwa miaka 30 hadi sasa toka mwaka 1995.
“Nina dhamira ya dhati kulitumikia Jimbo la Isimani Lukuvi mwenyewe alitangaza kuwa hatagombea tena mwaka 2025 hivyo ni muda sasa wa vijana kuongoza yeye abaki kuwa mshauri na endapo akagoma kustaafu kwa heshima basi tutamstaafisha” amesema Kiswaga.
Leave a Reply