Amad Diallo, winga wa Manchester United mwenye umri wa miaka 22, amekubali kusaini mkataba mpya na klabu hiyo utakaomuweka Old Trafford hadi Juni 2030.
Mkataba huu mpya hauna kipengele cha kuongeza muda zaidi.
Diallo alikataa ofa kutoka kwa vilabu viwili vikubwa, akionyesha nia yake ya kuendelea na Manchester United.
Kwa Mara ya kwanza alitua United akitokea Atalanta mnamo Januari 2021, Diallo amekuwa na maendeleo makubwa, ikiwa ni pamoja na vipindi vya mkopo katika timu ya Rangers na Sunderland.
Katika msimu huu, Diallo amekuwa na mchango mkubwa chini ya kocha mpya wa Klabu hiyo, Ruben Amorim, akifunga mabao na kutoa pasi za mabao katika mechi za hivi karibuni.
Got a Questions?
Find us on Socials or Contact us and we’ll get back to you as soon as possible.