Diamond Alipwa Zaidi Ya Davido Birthday Ya Bilionea Wa Ghana.

Kwa mujibu wa tovuti mbalimbali nchini Ghana, zimeibuka ripoti kuhusu kiasi cha fedha kinachodaiwa kulipwa kwa wasanii waliotumbuiza kwenye sherehe ya kifahari ya bilionea wa nchi hiyo, Richard Nii Quaye. Sherehe hiyo ya siku yake ya kuzaliwa ilifanyika Jumamosi, Machi 22, na ilihudhuriwa na mastaa wakubwa wa muziki kutoka Afrika Mashariki, Magharibi na kwingineko.

Katika taarifa hizo, ambazo zimeambatana na screenshot zinazoonyesha malipo ya wasanii, imebainika kuwa msanii kutoka Tanzania, Diamond Platnumz, ndiye aliyelipwa kiasi kikubwa zaidi kuliko wasanii wengine wote waliotumbuiza kwenye hafla hiyo. Inadaiwa kuwa alilipwa dola 600,000, sawa na takribani shilingi bilioni 1.5 za Kitanzania.

Wasanii wengine waliotumbuiza na malipo yao yanayodaiwa kulipwa ni:

• Davido 🇳🇬 – Dola 500,000 (Tsh bilioni 1.3)

• Sarkodie 🇬🇭 – Dola 200,000 (Tsh milioni 532.2)

• Stonebwoy 🇬🇭 – Dola 200,000 (Tsh milioni 532.2)

• King Promise 🇬🇭 – Dola 120,000 (Tsh milioni 319.3)

Ripoti hizi zimezua gumzo kubwa mitandaoni, huku mashabiki wakijadili viwango vya malipo ya wasanii wao pendwa na thamani yao katika tasnia ya burudani barani Afrika. Hata hivyo, mpaka sasa, hakuna uthibitisho rasmi kutoka kwa waandaaji wa hafla hiyo au wasanii wenyewe kuhusu malipo hayo yanayodaiwa.