Mkurugenzi wa Makampuni ya Wasafi, Nasibu Abdul Juma Diamond Platnumz , ametangaza nafasi za ajira katika kampuni zake mbalimbali, ikiwemo Wasafi TV, Wasafi FM, WCB Wasafi, Wasafi Soap, na Wasafi Bet.
Diamond Platnumz kupitia tangazo lake kwenye mtandao wa Instagram ameeleza kuwa, wanahitaji watu wenye ujuzi na uwezo wa kufanya kazi katika nafasi zifuatazo:
- Idara ya Fedha (Finance)
- Meneja Masoko na Mauzo (Marketing and Sales Manager)
- Mahusiano ya Umma (Public Relations – PR)
- Mkuu wa Ubunifu (Head of Creativities)
- Mameneja wa Wasanii (Artist Managers)
- Graphics Designers
- Social Media Managers
- Waandaaji wa Maudhui ya Wasanii (Artist’s Content Creators)
- Videographers
- Wapiga Picha (Photographers)
- Wapiga Vyombo vya Muziki (Drummer, Guitarist, Bassist, Keyboardist
Waombaji wote wenye sifa wanatakiwa kufika katika makao makuu ya Wasafi Media yaliyopo Mbezi Beach, Dar es Salaam, siku ya Jumamosi, tarehe 5 Aprili 2025, kuanzia saa nne asubuhi. Waombaji wanapaswa kuwasilisha CV zao.
Diamond Platnumz amesisitiza kuwa, wanahitaji watu wenye uwezo mkubwa wa kufanya kazi na wenye ubora. “Kama unajua huna uwezo wa kufanya kazi kwa ubora tunaohitaji, tafadhali usifike kabisa,” alisisitiza.
Leave a Reply