Diamond Platnumz Aandika Historia Kwa Kufikia Streams Zaidi Ya Milioni 500 Kwenye Boomplay!

Msanii wa muziki kutoka Tanzania, Diamond Platnumz, ameandika Historia Kwa Kufikia Streams Zaidi Ya Milioni 500 Kwenye Boomplay! Diamond Platnumz amefanikisha hatua kubwa kwa kuvuka streams zaidi ya milioni 500 kwenye Boomplay, na kuwa msanii wa kwanza kutoka Afrika Mashariki na Kusini kufikia rekodi hii.

Diamond Platnumz Aandika Historia Kwa Kufikia Streams Zaidi Ya Milioni 500 Kwenye Boomplay!
Diamond Platnumz Aandika Historia Kwa Kufikia Streams Zaidi Ya Milioni 500 Kwenye Boomplay!

Diamond Platnumz, ambaye ameendelea kuwa miongoni mwa wasanii wenye ushawishi mkubwa barani Afrika, ameweka alama katika tasnia ya muziki kupitia nyimbo zake nyingi maarufu. Kuanzia #Kamwambie, #NumberOne, #MarryYou, #Jeje, #Waah, hadi wimbo wake wa hivi karibuni #Komasava, ameendelea kutoa muziki unaovuma ndani na nje ya bara la Afrika.

Mashabiki wanaweza kuendelea kufurahia nyimbo zake kupitia Boomplay, jukwaa linaloongoza kwa usambazaji wa muziki wa kidijitali. Kupitia rekodi hii, Diamond Platnumz anaendelea kuonesha ukuaji wa muziki wa Afrika katika soko la kimataifa.