Dk. Wilbroad Slaa Aachiwa Huru na Mahakama ya Kisutu

Dar es Salaam – Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemwachia huru Mwanasiasa Dk. Wilbroad Slaa (76) baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP) kuwasilisha nia ya kutokuendelea na kesi hiyo.

Dk. Slaa alikuwa akikabiliwa na mashtaka ya kusambaza taarifa za uongo kupitia mtandao wa kijamii wa X (zamani Twitter), kinyume na kifungu cha 16 cha Sheria ya Makosa ya Kimtandao.

Uamuzi huo ulitolewa leo mbele ya Hakimu Mfawidhi Franco Kiswaga, ambapo mahakama ilizingatia maombi yaliyowasilishwa na upande wa Jamhuri pamoja na kesi ya msingi. Baada ya kusikiliza hoja hizo, Hakimu Kiswaga alitangaza kuwa Dk. Slaa hana kesi ya kujibu na hivyo kumwachia huru.

.