Dkt. Migiro awataka Viongozi wa Juu CCM wasiwe ‘Watu wa Amri tu’

Katibu Mkuu wa CCM Balozi Dkt. Asha Rose Migiro ametoa agizo kwa Viongozi wa Juu wa CCM kuacha utaratibu wa kutoa amri kutoka juu kushuka chini badala yake wanatakiwa washuke chini kuanzia ngazi ya mashina na kata ili kujua matatizo ya wananchi na kero zao ili kuzitatua kwa shabaha ya kuendelea kukiimarisha chama hicho.

Dkt Migiro ametoa angalizo hilo leo Januari 7, 2025 Jijini Dar es Salaam katika kikao kazi cha CCM Wilaya ya Temeke inayojumuisha majimbo matatu yakiwa Temeke, Mbagala na Kigamboni.

“Ninatoa wito Kwa Viongozi wa matawi na kata kuwa wazi na kushirikiana na uongozi wa juu ili utekelezaji wa maazimio ya CCM na ilani Viweze kutimia Kwa wakati” amesema Dkt Migiro.

Kwa upande wake Mlezi wa CCM mkoa Dar es Salaam ambaye pia ni Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama hicho Kenani Kihongosi amesisitiza Watanzania kuendelea kuilinda Amani ya Nchi, ikiwa ni tunu ya Taifa kwa Sasa.

Wakizungumza na Wasafi Media Baadhi ya Wajumbe na Mabalozi wa mashina wametoa maoni yao juu ya maagizo ya Dkt Migiro na uelekeo wa Chama cha Mapinduzi (CCM).

@Mwinyi_tza