Dkt. Mwinyi kuunda Tume maalum kufuatilia mwenendo wa fidia, “aahidi kusimamia haki za wananchi

Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi, Dk.Huseein Ali Mwinyi ameahidi kuunda Tume ya kutathimini fidia zote zilizotayarishwa kwa ajili ya wananchi wa maeneo ya Dimani, Bweleo, Fumba na vijiji jirani ili kuhakikisha kila mwananchi anapata haki yake.

Dk.Mwinyi ameeleza hayo wakati akizungumza na wazee wa Dimani na wananchi wa Dimani, Bweleo, Kombeni, Nyamanzi na Fumba katika uwanja wa mpira Dimani wilaya ya Magharibi ‘B’ Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.

Amesema tume hiyo itakwenda kuhakiki miradi ya iliyolalamikiwa ikiwemo Chuo cha IIT madrasa, uwanja wa mpira wa Afcon na mradi wa Fumba Port ili kuona wananchi wanaliowa fidia stahikikwa mujibu wa maeneo yao