Dodoma, Tanzania: Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo tarehe 17 Januari 2025, ameongoza kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, kilichofanyika jijini Dodoma.

Kikao hiki ni sehemu ya maandalizi ya Mkutano Mkuu Maalum wa CCM unaotarajiwa kufanyika tarehe 18 na 19 Januari 2025, jijini humo.
Mkutano huo maalum unalenga kujadili masuala mbalimbali ya maendeleo ya chama na taifa, pamoja na kuweka mikakati ya kuimarisha utendaji wa CCM kuelekea uchaguzi ujao na maendeleo ya kitaifa.

Moja ya ajenda muhimu za Mkutano Mkuu Maalum ni kupata mrithi wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa chama, iliyokuwa ikishikiliwa na aliyekuwa Makamu Mwenyekiti Abdulrahman Kinana.




Leave a Reply