Drake Aifuta Kesi Yake Dhidi Ya UMG na Spotify.

Drake ameifuta rasmi kesi aliyofungua dhidiya Universal Music Group (UMG) na Spotify. Kesi hiyo ilihusisha madai ya kudanganya hesabu za streams za wimbo wa Kendrick Lamar, Not Like Us, ambapo Drake alidai kwamba UMG na Spotify walikuwa wakishirikiana kuuufanya wimbo huo unonekane umesikilizwa mara nyingi.

Kama ilivyoripotiwa, Drake na timu yake ya kisheria walikutana na wawakilishi wa UMG na Spotify Jumanne, Januari 14, 2025, na kufikia makubaliano ya kuondoa kesi hiyo bila gharama kwa pande yoyote.

Uamuzi wa Drake kuondoa kesi umeshangaza wengi, na sasa maswali yanajitokeza kuhusu sababu halisi ya hatua hii.