Elissa: Malkia Wa Muziki Wa Kiarabu.

Elissar Zakaria Khoury(52), maarufu kama @elissazkh 🇱🇧, ni mmoja wa wasanii wakubwa kutoka Lebanon, aliyeanza muziki mwishoni mwa miaka ya 90 na kupata mafanikio kupitia albamu zake “Ayshalak” na “Ahla Dounya”.

Wimbo wake “Halali” ni mojawapo ya kazi zake zilizothibitisha uwezo wake mkubwa wa kimuziki, huku akibaki kuwa malkia wa muziki wa Kiarabu, akitoa nyimbo zinazofanya vizuri duniani kote.

Mwaka 2018, Elissa alitangaza Kupata Ugonjwa Wa saratani ya matiti, na baada ya kupona, alitoa wimbo “Ila Kol Elli Bihebbouni” kusherehekea ushindi wake dhidi ya ugonjwa huo.

Mbali na muziki, Elissa ni mpigania haki za kijamii na kisiasa nchini Lebanon, akitetea haki za wanawake, kukosoa hali mbaya ya uchumi, na kuzungumzia masuala nyeti kama ugaidi. Msimamo wake umeleta changamoto, lakini hajawahi kukaa kimya.

Licha ya vikwazo, Elissa ni mmoja wa wasanii wa Kiarabu wenye streams nyingi zaidi duniani, Amepata tuzo kadhaa, ikiwemo World Music Award kwa kuwa msanii wa Kiarabu aliyefanikiwa zaidi kimuziki. “Halali” ni moja ya nyimbo zilizowafanya mashabiki wengi kumpenda kutokana na ujumbe wake wenye hisia na uimbaji wake wa kipekee. 🎶🔥