Elon Musk Hapokei Simu, Hatoi Pesa Za Matibabu.

Aliyewahi Kuwa Mwanamke Wa Elon Musk, Ambaye Pia Ni Mama Wa Watoto Wake “Grimes”, Amemlalamikia Tajiri Huyo Namba Moja Duniani Kupitia Mtamdao Wa X Kuwa Hapokei Simu Zake Wala Hajibu Meseji Zake Pale Anapomtafuta Kwaajili Ya Matibabu Ya Mtoto Wao.

“Ninasikitika kufanya hivi hadharani lakini sio sawa kuendelea kupuuza hali hii, Ikiwa hutaki kuzungumza nami unaweza tafadhali kuteua au kuajiri mtu anayeweza ili tuweze kusonga mbele katika kutatua hii dharura, Elon”.

Hata Hivyo Baada Ya Grimes Kuulizwa Na Baadhi Ya Wadau Mtandao kuhusu tatizo la mtoto, Grimes alijibu, “Sitatoa maelezo zaidi, hapokei simu, sms au emails zangu, nahitaji kuwasiliana nae sasa hivi, ili kumwokoa mtoto lasivyo atapata madhara ya muda”.