Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Judith Kapinga amelitaka Baraza la Ushindani FCT kufanya maamuzi kwa haraka kwa kuzingatia Sheria na Weledi
amesema Baraza la Ushindani (FCT) linaendelea kuwa nguzo muhimu kwa wafanyabiashara nchini, hususan katika usuluhishi wa migogoro ya kibiashara, na amelitaka kuendelea kulinda misingi ya weledi, sheria na kanuni katika utendaji wake.
Akizungumza Novemba 25, 2025 wakati wa ziara yake katika Ofisi za Baraza Hilo, Waziri Kapinga amesema masuala ya kisheria na kanuni hayapaswi kuwa kikwazo katika utekelezaji wa shughuli za kibiashara ambazo haziwezi kusubiri.
Aidha, amesisitiza kuwa iwapo kuna kanuni zinazohitajika kuboreshwa, FCT inapaswa kuchukua hatua mapema ili kuendana na mabadiliko ya mazingira ya biashara ili kuchochea mazingira wezeshi ya uwekezaji na biashara.
Aidha, amelipongeza Baraza Hilo kwa kuongeza kasi katika kushughulikia mashauri ya kibiashara ili kuwasaidia wafanyabiashara.
Hata hivyo Kapinga ameridhishwa na hatua ya FCT kuanzisha Mfumo wa kusimamia kesi na kuwatkaa wauboreshe zaidi ili kuwezesha mashauri kusikilizwa kwa njia ya mfumo, na akaongeza kuwa maboresho hayo yaanze kutumika katika miji mikubwa ambapo biashara zinafanyika sana ikiwemo Arusha, Mbeya, Mwanza na Tanga.
Aliongeza kuwa uboreshaji wa mifumo ya kidijitali utapunguza gharama kwa wadau na kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma, sambamba na kuifanya FCT kuwa karibu zaidi na wafanyabiashara wanaohitaji huduma zake.















Leave a Reply