Filamu Ya ‘John Wick 5’ Ipo Kwenye Maandalizi, Keanu Reeves Kurudi Tena!.

Imethibitishwa kuwa Muendelezo Wa Filamu Za John Wick, ‘JOHN WICK 5’ Sasa Ni rasmi Ipo Kwenye utayarishaji. Keanu Reeves atarudi katika nafasi yake kama John Wick, Chad Stahelski Ataendelea kuwa mwongozaji (Director), Huku Basil Iwanyk pamoja na Erica Lee wakiwa kama watayarishaji (Producers).

Swali la wengi lilikuwa kama Keanu Alishamalizana na filamu hii, kwani John Wick: Chapter 4 ilionekana kama hitimisho kwa Uhusika wake, hasa baada ya filamu kumalizika Kwa Utata Juu Ya Kifo Chake.

Machi 2023 Muongozaji wa Filamu ya ‘John Wick : Chapter 4, Chad Stahelski Alisema mhusika mkuu wa filamu hii Ambaye Ni Keanu Reeves huwenda akapumzika kwenye uandaaji wa Chapter 5 kwa muda mpaka watakapoona mapokezi ya Chapter 4, Hivyo Baada Ya Kupata Mapokezi Makubwa Na Mashabiki Kudai Muendelezo Sasa Imethibitishwa John Wick (Kean Reeves) Atarudi Tena Kwenye John Wick 5 Ambayo Inafanyiwa Maandalizi Kwa Sasa.