Guardiola: Man City imerudi kwenye ubora wake

Kocha wa Manchester City Pep Guardiola (54) amesema kikosi chake kimerejea kwenye makali yake ya zamani kufuatia kipigo kiziti cha mabao 6-0 walichokishusha kwa Ipswich Town siku ya jana, Jumapili Januari 19, 2025 na kuwapandisha hadi nafasi nne katika msimamo wa Ligi Kuu ya Uingereza.

“Tumefurahiya sana, tumerudi kwenye kile kiwango ambacho kinaipambanua hii kama timu bora kwa muda wa miaka mingi sasa.

“Nimefurahishwa sana na alama hizo tatu na kupanda katika nafasi ya kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa kwa msimu ujao,” Guardiola aliiambia Sky Sports.