Gwiji Wa Mieleka Hulk Hogan Afariki Dunia.

Gwiji wa mieleka Hulk Hogan ameripotiwa kufariki Dunia akiwa na umri wa miaka 71, kwa mujibu wa taarifa kutoka TMZ Sports. Inasemekana kuwa Wahudumu Wa dharura Waliitwa nyumbani kwake huko Clearwater, Florida, mapema Alhamisi asubuhi, Kufuatia Tukio La “cardiac arrest” (mshituko wa moyo).

Mashuhuda walimwona Hogan akitolewa nyumbani Kwake Na machela (stretcher) na kuingizwa kwenye ambulance. Ripoti Zinadai Kuwa Hogan alikimbizwa hospitalini ambako alitangazwa rasmi kuwa amefariki dunia.