Haki za uchapishaji na utangazaji za marehemu The Notorious B.I.G. zinakaribia kuuzwa kwa thamani inayokadiriwa kati ya dola milioni 100 hadi 150. Kwa mujibu wa taarifa za The Hollywood Reporter, mnunuzi anayeongoza katika mazungumzo haya ni Primary Wave, kampuni inayojihusisha na haki za muziki na usimamizi wa wasanii.
Kwa mujibu wa vyanzo vya habari, makubaliano haya yatakuwa na asilimia 50 ya haki za uchapishaji na master za marehemu Biggie, pamoja na haki za utangazaji, ikiwa ni pamoja na picha, sauti na mistari muhimu ya nyimbo zake maarufu.
Tangazo hili linakuja siku chache baada ya kifo cha Voletta Wallace, mama yake Biggie ambaye alikuwa msimamizi mkuu wa kazi zake. Voletta ameendelea kuhakikisha urithi wa mwanaye unabaki hai tangu kifo chake mwaka 1997, na mchango wake katika kuhifadhi kazi za Biggie umetambuliwa na kuheshimiwa na mashabiki wa hip-hop duniani kote.
Hili linakuja pia miezi michache baada ya Sean “Diddy” Combs kurejesha haki za uchapishaji kwa wasanii wa lebo yake ya Bad Boy Records, ikiwa ni pamoja na kazi za Biggie.
Makubaliano haya yanatarajiwa kufungwa ndani ya wiki chache zijazo.
Got a Questions?
Find us on Socials or Contact us and we’ll get back to you as soon as possible.