Hali ya Siasa na Utekelezaji wa Demokrasia imeendelea Kuimarika Tanzania

Waziri mkuu Mhe. Kassim Majaliwa amesema hali ya siasa na utekelezaji wa Demokrasia imeendelea kuimarika Nchini kutokana na maboresho ya mifumo na jitihada mbalimbali zinazofanywa kwa makusudi na Serikali


Waziri mkuu amesema Moja ya jitihada hizo ni marekebisho ya sheria mbalimbali kwa lengo la kuimarisha utawala wa demokrasia hapa nchini.

“Bunge lako Tukufu lilitunga Sheria ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Na. 1 ya Mwaka 2024; Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani Na. 2 ya Mwaka 2024 na kufanya Marekebisho ya Sheria ya Vyama vya Siasa Sura ya 258.”

“Serikali kwa upande wake tayari imeshakamilisha utungaji wa Kanuni za Sheria ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi.” – Waziri Mkuu Majaliwa ameeleza hayo wakati anawasilisha bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha 2025/2026 leo Aprili 9, 2025 Bungeni jijini Dodoma ambapo