Heche asema CHADEMA haitarudi nyuma licha ya Lissu kukamatwa

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa, John Heche, amesema kuwa chama hicho hakitorudi nyuma katika harakati zake za kudai mabadiliko ya mifumo ya uchaguzi nchini, licha ya Mwenyekiti wa Chama hicho Tundu Lissu kuendelea kuwa mahabusu.

Heche amesisitiza kuwa CHADEMA itaendelea kusonga mbele na hakitishwi na kukamatwa kwa viongozi wake huku akiwataka wanachama kuendelea na harakati hizo bila woga.

Aidha, Heche ametoa msimamo wa chama hicho kuhusu ushiriki wao katika uchaguzi mkuu ujao, akisema kuwa CHADEMA hakiko tayari kushiriki katika uchaguzi huo kama hakutakuwa na mabadiliko ya mifumo ya uchaguzi yanayodaiwa na chama hicho kwa muda mrefu.