Idadi ya Watu wanaodai Kutapeliwa na Nicole Yaongezeka

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro, amesema kuwa idadi ya watu wanaojitokeza wakidai kutapeliwa na msanii Joyce Mbaga, maarufu kama Nicole Berry, inaendelea kuongezeka, huku kiwango cha fedha kilichotapeliwa nacho kikiongezeka pia.

Nicole Berry alikamatwa Machi 3, 2025, Anatuhumiwa kujipatia zaidi ya Sh100 milioni kwa njia za udanganyifu, kwa kuunda vikundi vya upatu kwenye mitandao kinyume na sheria.

Kamanda Muliro ametoa wito kwa wananchi kuwa makini wanapotaka kufanya biashara zinazopitia mitandao, hasa magrupu ya upatu, kwani yanaweza kuwa na udanganyifu.