INEC yakamilisha zoezi la Uteuzi wa Wagombea Urais

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imefunga rasmi dirisha la kupokea fomu za wagombea wa Urais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ikiashiria hatua muhimu kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2025. Jumla ya vyama 17 vya siasa vimerudisha fomu zao, huku Chama cha ACT-Wazalendo kikielezwa kukosa sifa kwa mujibu wa kanuni za Tume.

Baada ya kukamilika kwa zoezi la uteuzi wa wagombea wa Kiti cha Rais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo tarehe 27 Agosti, 2025 saa 10:00 Alasiri, fomu za uteuzi zilibandikwa nje ya Ofisi za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi.

Vyama vilivyorejesha fomu ni CCM, NRA, AAFP, MAKINI, NLD, UPDP, ADA- TADEA, UMD, TLP, CCK, CHAUMMA, DP, SAU, CUF, ADC, UDP, na NCCR-Mageuzi.