JKT Yasema Huwafundisha Vijana utimamu wa Mwili na Uzalendo, Sio Mafunzo ya Kijeshi

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Rajabu Mabele, amefafanua kuwa JKT halilengi kuwafundisha vijana mafunzo ya kijeshi bali linawajengea utimamu wa mwili, uzalendo na maadili.

Meja Jenerali Mabele amefafanua kuwa mafunzo ya kijeshi ni yale maalum yanayowaandaa vijana kwa ajili ya uwanja wa vita, tofauti na JKT ambayo inalenga kuwalea vijana kuwa wazalendo kwa taifa lao, kuwa na maadili mema katika jamii, na uwezo wa kujitegemea.

Kwa upande wao, baadhi ya wanafunzi wa mwaka wa kwanza na wa pili wa UDOM waliopitia mafunzo ya JKT, wameeleza jinsi mafunzo hayo yalivyowapa ujasiri na uzalendo. Pia wamesema yamewasaidia kupata fursa mbalimbali, hususan katika Serikali ya Wanafunzi wa UDOM.

Naye Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) anayeshughulikia taaluma, utafiti na ushauri elekezi, Profesa Razack Lokina, amepongeza mchango wa JKT katika kudumisha utulivu chuoni hapo. Amesema tangu vijana waliopitia mafunzo ya JKT waanze kuunda vikundi vyenye mienendo mizuri kwa jamii, wanafunzi wamekuwa wasikivu na wengi wamebadilika tabia na