Jumuiya ya Wazazi CCM Temeke Yawagusa Yatima, Wasiojiweza

Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Temeke, Jana Machi 7 imepata Iftar pamoja na makundi mbalimbali wakiwemo yatima kutoka vituo viwili vilivyopo maeneo ya Kijichi, Dar es salaam na kuwakabidhi fedha taslim za kujikumu na kanzu na mabaibui ambayo watavalia sikukuu ya Eid

Aidha mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Temeke, Ndugu Hamisi Slim Hamisi ameikumbusha jamii kujitoa kwa wasiojiweza hususani katika kipindi hiki cha mfungo wa Ramadhan

Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Mbagala Mhe. Kakulu Burchard Kakulu ambaye ndiye aliyekuwa mgeni rasmi amesema kuwa kitendo walichofanya Jumuiya ya Wazazi wilaya ya Temeke ni wazi kuwa wanatambua majukumu yao na lengo la jumuiya hiyo kuanzishwa