Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linashirikiana na Jeshi la India pamoja na majeshi mengine ya nchi rafiki katika maandalizi ya Zoezi la Kijeshi la Wanamaji la ‘Africa India Key Maritime Engagement (AIKEYME)’.
Taarifa iliyotolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania, Kanali Gaudentius Gervas Ilonda imeeleza kuwa Zoezi hili litafanyika katika Bandari ya Dar es Salaam na baharini kuanzia tarehe 13 Aprili, 2025 hadi tarehe 18 Aprili, 2025.
Lengo kuu la zoezi hili ni kuongeza weledi na uelewa wa pamoja katika kukabiliana na matishio mbalimbali ya kiusalama baharini, ikiwa ni pamoja na uharamia.
JWTZ inawaarifu wananchi kuwa kutakuwa na ongezeko la matumizi ya Meli Vita katika kipindi hiki na hivyo hawapaswi kuwa na taharuki.
Leave a Reply