Kampeni Ya Msaada Wa Kisheria Kutatua Migogoro Katika Sekta Ya Madini Geita.

Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Martine Shigela amewahamasisha wananchi wa Mkoa huo kujitokeza kwa wingi kutumia fursa ya kampeni ya kitaifa ya msaada wa kisheria ya Mama Samia (Mama Samia Legal Aid Campaign) ili kusikilizwa na kupatiwa msaada huo.

Mhe. Shigela ameyasema hayo leo Januari 26, wakati wa uzinduzi wa Kampeni hiyo kwa niaba ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko.

“Tuna kila sababu za kumshukuru Rais wetu mpendwa kwa kutuletea msaada huu sisi wananchi wa Geita niwaombe mjitokeze ili mpate msaada wa migogoro inayowakabili hasa katika sekta ya madini ” Ameongeza Mhe. Shigela

Naye mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Alfred Dede amewaeleza wananchi hao kuwa baada ya uzinduzi kampeni hiyo itaendelea kwa siku tisa katika Halmashauri zote za Mkoa wa Geita kuanzia Januari 27, 2025.