Harry Kane (31), ambaye ni mshambuliaji wa Uingereza na klabu ya Bayern Munich, amefikisha jumla ya mabao 71 katika timu yake ya Taifa ya Uingereza na kuendelea kuwa mfungaji wa muda wote wa Taifa hilo.
Alianza kuchezea timu ya taifa ya Uingereza mnamo Machi 2015 katika ushindi wa 4-0 dhidi ya Lithuania, ambapo alifunga bao lake la kwanza baada ya sekunde 80 tu akiwa uwanjani.
Kane amecheza mechi 105 na kufunga mabao 71 kwa timu ya taifa ya Uingereza, akimfanya kuwa mfungaji bora wa muda wote wa taifa hilo.
Machi 2023 alivunja rekodi ya mabao 53 iliyowekwa na Wayne Rooney kwa kufunga penalti dhidi ya Italia katika mechi ya kufuzu Euro 2024.

Tangu wakati huo, ameendelea kuongeza idadi ya mabao yake, akifikia bao la 71 katika mechi dhidi ya Latvia katika mchezo uliopigwa Jana Machi 24, 2025.
Mchango wake katika mashindano makubwa na uongozi wake umeifanya Uingereza kuwa miongoni mwa timu tishio duniani. Kwa mabao 71 katika mechi 105, Kane ameonyesha kiwango cha juu cha ufanisi na kujitolea kwa taifa lake.
Got a Questions?
Find us on Socials or Contact us and we’ll get back to you as soon as possible.