Kesi ya Rufaa inayowakabili warufani wanne, wakiwemo askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Jeshi la Magereza, ambao walihukumiwa kifungo cha maisha jela na faini ya shilingi milioni moja kila mmoja kwa kosa la kumbaka na kumuingilia kinyume cha maumbile binti mkazi wa Yombo Dovya jijini Dar es Salaam, imeahirishwa hadi Juni 9, 2025, katika Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma.
Warufani hao, ambao walihukumiwa katika kesi ya jinai Namba 23476 ya mwaka 2024, ni MT 140105 Clinton Damas maarufu kama Nyundo, askari wa Magereza C. 1693 Praygod Mushi, Nickson Jackson, na Amin Lema. Wote walikutwa na hatia ya kumbaka na kumuingilia kinyume cha maumbile binti huyo.
Akizungumza mara baada ya kuahirishwa kwa kesi hiyo, Wakili Mtetezi, Meshack Ngamando, amesema mwenendo wa kesi ni mzuri. Hata hivyo, amedai kuwa hati ya mashtaka ya kesi ya msingi ilikuwa na mapungufu mengi.
Wakili Ngamando ameongeza kuwa kesi hiyo itasikilizwa tena Juni 9, 2025, ambapo mapungufu mengine ya hati ya mashtaka ya kesi ya msingi yanatarajiwa kuonekana.
Leave a Reply