Kesi ya Lissu kupinga mashahidi wa Jamhuri kufichwa kuamuliwa Agosti 12



Uamuzi wa maombi ya mapitio yaliyofunguliwa na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu ya kuomba mahakama hiyo kufanya marejeo ya maombi ya Jamhuri kuficha baadhi ya mashahidi wake katika kesi ya uchochezi inayomkabili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu yamepangwa kutolewa Agosti 12, 2025.

Katika shauri hilo liloendelea leo Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, mbele ya Jaji Elizabeth Mkwizu, baada ya kusikiliza maombi yamleta maombi (Lissu) na majibu ya Serikali.

Jaji Mkwizu amesema siku hiyo pia atatoa uamuzi kuhusiana na malalamiko ya Lissu dhidi ya askari Magereza kumnyima fursa ya kuwasiliana na mawakili wake na kupewa nyaraka muhimu.

@hamisimguta
#WasafiDigital