Kesi ya Tundu Lissu kujadiliwa Bunge la Ulaya

Bunge la Ulaya limepanga kufanya mjadala wa dharura tarehe 7 Mei 2025, kujadili kesi ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, ambaye anakabiliwa na mashtaka ya uhaini na uchochezi nchini Tanzania.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwenye tovuti rasmi ya Bunge hilo, mjadala huo utaanza saa 13:00 hadi 22:00 (saa za Ulaya). Baada ya mjadala huo, wabunge wanatarajiwa kupiga kura juu ya azimio lenye kumbukumbu 2025/2690 (RSP) siku inayofuata, tarehe 8 Mei 2025.

Tundu Lissu alikamatwa Aprili 9, 2025 baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara huko Mbinga, Ruvuma na kufunguliwa mashtaka ya uhaini pamoja na tuhuma za uchochezi ambayo yanaweza kusababisha hukumu ya kifo