Kijana aliyefahamika kwa jina la Yona Angres, anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 34 na 40, amefariki dunia katika banda la burudani lililopo mtaa wa Sawe, kata ya Maisaka, mjini Babati, mkoa wa Manyara akidaiwa kuwa alikunywa Pombe Kupita Kiasi.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Sawe, John Paulo, chanzo cha kifo hicho kinadaiwa kuwa ni unywaji wa pombe kupita kiasi bila kula chakula.
Jeshi la Polisi lilifika eneo la tukio na kuuchukua mwili wa marehemu kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
Wakazi wa mtaa huo wameeleza masikitiko yao juu ya tukio hilo na kutoa wito wa kuimarisha juhudi za uhamasishaji juu ya madhara ya unywaji wa pombe kupindukia.
Leave a Reply