Kila mmoja ana Wajibu wa Kuilinda na Kuijenga Tanzania – Dkt. Mpango

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Philip Mpango, amewataka watanzania kumuenzi baba wa Taifa mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa kusimamia misingi mikuu aliyotuachia ikiwa ni pamoja na kulinda uhuru wetu pamoja na kulinda amani tuliyonayo kwa dhati.

Dkt Mpango ameeleza hayo kwenye sherehe za kilele cha mbio za mwenge wa uhuru mwaka 2025 na kumbukizi ya miaka 26 ya kifo cha Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere, ambapo amesema ni lazima tuendelee kukemea mmomonyoko wa maadili kwa vijana ikiwemo Rushwa na Ufisadi vitu ambavyo baba wa taifa alivipinga kwa vitendo, nakwamba tusipofanya hivyo kwa dhati kuna hatari kubwa ya taifa letu kusambaratika.

Mhe. Ridhiwani Kikwete ni Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana Ajira Na Watu wenye ulemavu, amesema mwenge wa uhuru kwa mwaka 2025 umetembelea miradi ya maendeleo 1382 ikiwa na Thamani ya Trilioni 2.9 wakati kipaombele ikiwa ni secta ya Elimu,Afya,Maji,Barabara na uwezeshaji vijana kiuchumi.

Kwanupande wake kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa mwaka 2025 Ndg.Ismail Ali Ussi ameeleza baadhi ya mambo ambayo wameyabaini katika miradi ikiwa ni pamoja na kumuomba Mhe. Rais kushughulikia jambo la baadhi ya taasisi kuzuia miradi yao kupitiwa na mwenge wa uhuru.