Kim Kardashian aguswa na bidii za wazima moto Los Angeles

Kim Kardashian, akishuhudia moto mkubwa unaoteketeza maeneo ya Los Angeles, ameeleza hisia zake za uchungu na kutoa heshima kwa juhudi za wazima moto, hasa wale walioko gerezani. Kupitia ujumbe aliouchapisha, Kim aliandika:

“Kwenye moto yote mitano huko Los Angeles, kuna mamia ya wazima moto walioko gerezani, wakihatarisha maisha yao kutuokoa. Wapo kwenye moto wa Palisades na Eaton huko Pasadena wakifanya zamu za saa 24.

Malipo yao ni sawa na bure, wanahatarisha maisha yao, wengine wamekufa, ili kuthibitisha kwa jamii kwamba wamebadilika Nawaona kama mashujaa.”

Kim alisisitiza mchango wa hawa wazima moto walioko gerezani, ambao licha ya malipo duni, wamejitolea kupambana na moto ili kuokoa maisha na mali za watu. Wengi wa wazima moto hawa wanatumia nafasi hii kuonyesha kwamba wamebadilika na sasa wanahudumia jamii kama wahudumu wa dharura wa mstari wa mbele.