Kinachoendelea Chelsea, Bayern ni ‘nipe nikupe’

Kocha wa Chelsea, Enzo Maresca amesema kuwa mchezaji wake, Christopher Nkunku hajasema kama anataka kuondoka ndani ya Chelsea licha ya kuwepo na taarifa kuwa Bayern wanamtaka kama mbadala wa Mathys Tel ambaye anatajwa kuwa kwenye rada za Chelsea.

“Nkuku hajaniambia mimi kwamba anataka kuondoka. Hatukuzungumza juu ya mustakabali wake,” amesema Maresca.