Serikali ya Tanzania imependekeza kuanzisha vyanzo mbadala vya mapato ili kupunguza nakisi ya kibajeti iliyotokana na kupungua kwa misaada kutoka nje. Hatua hii itafanyika kwa kufanya marekebisho katika sheria mbalimbali, ikiwemo kuongeza kodi kwenye michezo ya kubahatisha.
Marekebisho yaliyopendekezwa yataathiri Sheria ya Michezo ya Kubahatisha, Sura 41, kwa kuongeza kiwango cha kodi kwenye zawadi ya ushindi (Winning tax). Kwa sasa, kodi kwenye michezo ya kubashiri matokeo (sports betting) itaongezeka kutoka asilimia 10 hadi asilimia 15. Vilevile, kodi kwenye michezo ya kasino ya ardhini (land-based casino) itaongezeka kutoka asilimia 12 hadi asilimia 15.
Mapato yatakayoongezeka kutokana na marekebisho haya yamepangwa kugawa kwa ajili ya sekta muhimu za kijamii. Asilimia 70 ya mapato hayo itaelekezwa kwenye Mfuko wa Udhamini wa Kudhibiti UKIMWI (ATF), huku asilimia 30 iliyobaki ikipelekwa kwenye Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kwa Wote (NHIF).
Leave a Reply