Kouassi afanyiwa upasuaji kukaa nje ya uwanja wiki nne (4)

Meneja Habari na Mawasiliano wa Yanga Sc, Ally Kamwe amesema kuwa mchezaji wao Kouassi Yao amefanyiwa upasuaji kwenye mguu hivyo ataendelea kuwa nje ya uwanja kwa muda wa takribani wiki nne au wiki zisizozidi sita (6).

Aidha Kamwe amesema kuwa mchezaji Maxi Nzengeli anaendelea vizuri na majeraha aliyokuwa ameyapata hivyo ataanza mazoezi siku ya Kesho na wachezaji wengine kwa ajili ya mechi dhidi ya MC Alger siku ya Jumamosi, Januari 18, 2025.