Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limeyafunga makanisa sita ya Ufufuo na Uzima yaliyopo eneo la ZZK Mbalizi, Mtaa wa Mnadani Rujewa Wilaya ya Mbarali, Wilaya ya Chunya, Rungwe, Kyela na Jijini Mbeya.
Taarifa ya kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya SACP Benjamini Kuzaga amesema wameyafungia makanisa hayo Kufuatia tamko la serikali lililotolewa Juni 02, 2025 kupitia msajili wa jumuiya za kiraia nchini la kufunga makanisa ya Ufufuo na Uzima kutoendelea kutoa huduma katika matawi yake yote yaliyopo nchi nzima.
Sacp Kuzaga amesema Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linaendelea kufanya ufuatiliaji ili kubaini uwepo wa makanisa hayo na kuchukua hatua za kisheria.
Leave a Reply