Meneja wa Manchester City, Pep Guardiola (54) amesisitiza kuwa mchezo wa kesho wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya PSG wataibuka kidedea katika mchezo huo muhimu baada ya kurejesha ari yao kwenye mchezo uliopita wa Ligi Kuu kwa kuichabanga Ipswich mabao 6-0.
Kikosi cha Guardiola kiko katika nafasi ya 22 kwenye msimamo wa timu 36 za Ligi ya Mabingwa huku kukiwa na michezo miwili.
Vilabu 24 bora vitafuzu hatua ya mtoano ambapo klabu nane za kwanza zitatinga moja kwa moja hatua ya 16 na timu kutoka namba tisa hadi 24 zinakabiliwa na mechi za mtoano hivyo kuongeza zaidi ugumu wa mechi hiyo kwa Manchester City na PSG walioko nafasi ya 29.
“Tumebakisha michezo miwili na kama tutashinda yote tunafuzu, hata tukishinda moja pia uwezekano upo mkubwa.
“Lazima tupate alama kwa sababu tulijitengenezea matatizo sisi wenyewe, hasa kwa Feyenoord, hata mchezo tuliopoteza huko Lisbon.
“Lakini wakati huo tulikuwa na shida nyingi. Hatukuweza kushindana tunavyotaka kwa sababu nyingi,” amesema Pep Guardiola.
Got a Questions?
Find us on Socials or Contact us and we’ll get back to you as soon as possible.