Maofisa Wengine Saba wa LBL Wakamatwa Morogoro

Jeshi la Polisi mkoa wa Morogoro linawashikilia watu saba wakazi wa Wilaya ya Mvomero na Manispaa ya Morogoro Mkoani Morogoro wafanyakazi na wawakilishi wa kampuni ya Leo Beneth London (LBL) kwa tuhuma za kufanya biashara haramu ya fedha kwa njia ya mtandao bila ya kibali cha Benki kuu ya Tanzania (BOT) pamoja na kuhusika na utapeli.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro SACP Alex Mkama ameeleza kuwa kwakushirikiana na Benki Kuu BOT walifanya msako tarehe 18 Februari na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao ambao wamekuwa wakihusika na biashara mtandao yenye vinasaba na utapeli.

Waliokamatwa ni Jackson John(30) Mfanyabiashara, David Francis (35) Mkurugenzi wa kampuni ya LBL tawi la Morogoro, Boazi Amboniye (42)Mkurugenzi wa kampuni ya LBL tawi la Turiani, Kundi Msalaba(31) Mhasibu wa kampuniya LBL Moses Dugomela (22) Mshauri wa kisheria LBL, Isaya Paulo (25) Dereva wa kampuni hiyo na Baraka Sanga (32) Mfanyabiashara.