Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana ameeleza kuwa Mapato yatokanayo na shughuli za utalii yameongezeka kutoka Dola za Marekani bilioni 1.3 Mwaka 2021 hadi kufikia Dola za Marekani bilioni 3.9 Mwaka 2024 sawa na ongezeko la asilimia 200 kwa watalii wa kimataifa.
Akizungumza Bunge wakati akiwasilisha Bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2025/2026, Waziri Dkt. Chana ameeleza kuwa mapato yatokanayo na utalii wa ndani yameongezeka kutoka Shilingi bilioni 46.3 Mwaka 2021 hadi Shilingi bilioni 209.8 Mwaka 2024 sawa na ongezeko la asilimia 353.1.
Hatua hii imeifanya Tanzania kuwa nafasi ya tisa (9) duniani na kushika nafasi ya tatu (3) Barani Afrika kwa ongezeko la mapato ikilinganishwa na hali ilivyokuwa kabla ya UVIKO-19.
Waziri Dkt. Pindi Chana ameliomba Bunge liidhinishe jumla ya Shilingi Bilioni 359,982,271,000 ili Wizara hiyo iweze kutekeleza malengo na vipaumbele iliyojiwekea kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026.
Kati ya fedha hizo, Shilingi 254,232,349,000 kwa ajill ya Matumizi ya Kawaida na Shilingi Billioni 105,749,922,000 ni za Miradi ya Maendeleo.
Leave a Reply