Msanii Wa Bongo Fleva Nchini @mbosso_ Ameweka Wazi Kupona Kabisa Ugonjwa Wa Moyo Ambayo Alikuwa Akipambana Nao Kwa Miaka Yote .
Mbosso Kupitia Ukurasa Wake Wa Ameweka Wazi Hilo Kwa Kuandika: “Siku Ya juzi kuja Jana ilikuwa na masaa 12 hadi Kutimia 24 yenye hofu kubwa kwangu ambayo yameleta matoke Ya furaha na amani ya milele kwangu , Familia yangu na kwa Mashabiki zangu wote wa Mziki Wangu
Nilipata nafasi yakutibiwa na Madaktari bingwa kabisa wa Maswala Ya moyo kutokea nchini misri ( Egypt 🇪🇬) sambamba na Madaktari kutoka nyumbani hapa hapa Tanzania ndani ya Lisaa Moja Tu na kila kitu kukamilika
Kwa sasa Kijana Wenu nimepona kabisa ugonjwa wa moyo uliokuwa unanisumbua kwa kipindi cha miaka yote na Jana jioni nimeruhusiwa kuendelea na mapumziko nyumbani na baada Ya Wiki 1 niweze kuendelea na majukumu yangu ya kila siku .. ” – Mbosso

Hivi Karibuni CEO Wa Label Ya WCB Alithibitisha Msanii ‘Mbosso’ Kujitegemea Na Kuanza Kufanya Kazi Zake Mwenyewe
Got a Questions?
Find us on Socials or Contact us and we’ll get back to you as soon as possible.