Rais wa Kenya William Ruto ameongoza taifa hilo katika kuomboleza na kulaani vikali mauaji ya Mbunge wa Kasipul, Charles Ong’ondo Were, aliyepigwa risasi na kuuawa jioni ya Jumatano, (Aprili 30,2025) jijini Nairobi.
Rais Ruto ameitaka Idara ya Usalama kuchunguza tukio hilo kwa kina na kuhakikisha waliohusika wanakamatwa na kufikishwa mbele ya sheria. “Polisi wafanye uchunguzi wa kina kuhusu tukio hili. Waliohusika lazima wawajibishwe.”
Kwa mujibu wa mashuhuda, watu wawili waliokuwa kwenye pikipiki walimzingira mbunge huyo akiwa ndani ya gari lake. Mmoja wao alishuka na kumpiga risasi kwa karibu kabla ya kutoroka huku Dereva wake akijeruhiwa, Were alikimbizwa Hospitali ya Nairobi lakini alifariki alipofikishwa.
Spika wa Bunge la Kitaifa, Moses Wetang’ula, alimtaja Were kama kiongozi jasiri aliyekuwa na dhamira ya dhati ya kuwatumikia wananchi wake. “Alikuwa mtetezi asiyeogopa wa watu wa Kasipul, na kifo chake ni pigo kubwa kwa taifa lote,” alisema Spika.
@Barakadon_
#WasafiDigital
Mbunge auawa kwa Risasi Kenya, Rais Ruto asema waliohusika lazima wawajibishwe

Leave a Reply