Mbunge Nusrat Hanje atangaza Kuhamia CCM

Mbunge wa viti Maalumu kundi la Vijana kutoka Mkoa wa Singida kupitia CHADEMA Nusrat Hanje amewatangazia wananchi wa mkoa huo na Watanzania kwaujumla kuwa anahama chama hicho na kujiunga na Chama cha Mapinduzi.

Hanje ametoa kauli hiyo leo Mei 18, mwak huu wakati wa mkutano wa hadhara alioufanya viwanja vya stendi ya Zamani Ikungi mjini huku akisema kwa miaka mitano aliyodumu Bungeni ameiva na sasa anatafuta changamoto nyingine za kisiasa nje ya CHADEMA.

Amesema uamuzi huo wa kuhamia CCM ameufanya bila shinikizo lolote bali ameamua yeye mwenyewe baada ya kuona na kuridhishwa na mambo makubwa ya kimaendeleo anayo yafanya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa wananchi wa Singida.

Katika Mkutano huo pia Hanje amewataka wanaikungi kujitokeza kwa wingi kumuunga mkono kuhamia CCM kwa kuwa tayari changamoto zao na kero zao zinaweza kutatuliwa bila kusababisha vurugu wala machafuko.