Mdaiwa amuua mdai kisa shuka la Kimasai

Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro linamshikilia Justin Mogela Mizambo (29) mjasiriamali mkazi wa Kihonda kwa tuhuma za kusababisha kifo cha Hamis Rashid Msingi (21) mjasiriamali mkazi wa Ugogoni.

Tukio hilo lilitokea usiku wa Agosti 16, 2025, katika mtaa wa Ugogoni Kata ya Mafisa Manispaa ya Morogoro kufuatia ugomvi wa kudai shuka la kimasai ambalo marehemu alimpa kwa mkopo mtuhumiwa lakini hakulirudisha Katika ugomvi huo mtuhumiwa alimpiga marehemu shingoni kwa kitu chenye ncha kali na kusababisha kifo chake.

Aidha Jeshi la Polisi linafanya uchunguzi juu ya kifo cha Idd Hamza (32) mkulima mkazi wa Kijiji cha Mlumbilo Wilaya ya Mvomero aliyekutwa amefariki ndani ya chumba chake mnamo Agosti 16, 2025. Marehemu anadaiwa kujinyonga huku uchunguzi wa awali ukionyesha alikuwa akisumbuliwa na msongo wa mawazo kwa muda mrefubv kutokana na upweke na matatizo ya afya ya akili.

Jeshi la Polisi linatoa wito kwa jamii kuhimiza maridhiano mawasiliano na msaada wa kisaikolojia pale panapotokea migogoro ili kuepusha matukio ya uvunjifu wa amani na madhara makubwa kama haya.