Kwa mujibu wa ripoti mbalimbali, jaji ameamuru Kuwa Megan Thee Stallion na Roc Nation Lazima Wakabiliane na kesi ya madai kutoka kwa mpiga Picha ambaye anadai alilazimika kushuhudia tendo la ngono wakati megan akiwa kwenye Tour, jambo ambalo linapelekea kesi yake Hii kuendelea Mahakamani.
Mwezi April 2024 Emilio Garcia alifungua kesi ya madai ya kufanyiwa unyanyasaji wa kingono na Megan Thee Stallion wakati akimlazimisha atazame wakati anashiriki ngono na mwanamke mwenza kwenye gari na madai mengine ni kutolipwa malipo yake pale alipokuwa anafanya kazi kwa muda wa ziada.
Mr Emilio alikua mpiga picha binafsi wa rapa Megan kati ya mwaka 2018 mpaka Juni, 2023. Kesi hiyo ipo mahakama kuu mjini Los Angeles na hukumu ya kesi hiyo bado haijatolewa. Hata Hivyo Mawakili Wa Rapa Huyu Waliibuka Na Kupinga vikali madai yaliyofunguliwa na Mr. Emilio Garcia, na kusema kwamba madai hayo sio ya kweli hata kidogo na anatumika kumchafua jina mteja wao.
Got a Questions?
Find us on Socials or Contact us and we’ll get back to you as soon as possible.