Miili Miwili Yaopolewa Mgodi Uliotitia Shinyanga

Miili ya Wachimbaji wawili, Michael Ngelela (26) na Macha Shabani (43) wakazi wa Wilaya za Sengerema na Misungwi mkoani Mwanza imeopolewa katika Mgodi mdogo wa Nyandolwa mkoani Shinyanga katika ajali ya kutitia na kufukia Wachimbaji 25,ambapo mpaka sasa waliokolewa ni saba watatu wako hai na wanne wamepoteza Maisha.

Miili hiyo ya watu wawili ni kati ya watu 20 waliokuwa wamesalia chini imeopolewa leo Agosti 17, 2025 ikiwa ni siku ya 7 tangu mgodi huo utitie na kufukia taktibani watu 25 ardhini.

Wakizungumza wakaguzi wa Migodi Midogo wameelezea kuwa vikosi vya uokoaji vinaendelea na zoezi hilo la uokoaji katika duara namba 20 na 103 ambapo inasadikiwa kuwa na watu 18 waliofukiwa.

Nao baadhi ya watu ambao wanasubiri ndugu zao kuokolewa katika ajali hiyo wamepongeza serikali kwa kuongeza mitambo na timu za uokoaji huku wakiwa na matumaini ya kuwapata ndugu zao.