Miili ya Wanakwaya Sita (6)  waliofariki kwa ajali Yaagwa Same



Miili sita (6) ya wanakwaya wa kanisa la KKKT Same waliofariki kwa ajali ya gari siku ya jumapili, imeagwa leo ili kuwapa fursa ndugu kuzihifadhi siku ya kesho.

Miili hiyo imeagwa katika kanisa la KKKT dayosisi ya Pare, ambapo Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Nurdin Babu aliongoza waombolezaji kutoa heshima za mwisho

.

Akitoa salamu za pole, Nurdin Babu amesema Rais Samia Suluhu Hassan ametoa pole kwa kanisa huku akiwataka wawe na uvumlivu katika kipindi hiki kigumu.



Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Same Kaslida Mgeni amesema serikali inaendelea kutoa uangalizi wa karibu kwa majeruhi ambao wanaendelea na matibabu katika hospitali ya wilaya.

Mbunge wa jimbo la Same Magharibi David Mathayo amesema licha ya kutoa jeneza zote sita lakini akachangia kila familia ya wafiwa shilingi laki nne.