#TANZIA: Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, Mhe. Ester Mahawe amefariki dunia leo Januari 14, 2025 katika hospitali ya Rufaa ya kanda ya kaskazini -KCMC Mkoani Kilimanjaro alipokuwa anapatiwa Matibabu.
Taarifa ya kifo chake imetangazwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Mohamed Mchengerwa kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan
“Nimepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha Mkuu wa Wilaya ya Mbozi mkoani Songwe Mhe. Ester Mahawe. Kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ninatoa pole kwa familia, Mkuu wa Mkoa wa Songwe, wafanyakazi na wananchi wote wa wilaya ya mbozi, ndugu, jamaa na mafariki kwa msiba huu. Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi’ amesema waziri Mchengerwa.
Leave a Reply