Uongozi wa Klabu ya Yanga, umesema kuwa msimamo wa Klabu yetu juu ya mchezo namba 184 wa Ligi Kuu Msimu huu uko palepale kuwa hawatoshiriki kwenye mchezo huo kwa namna yoyote ile.
Taarifa hiyo imetolewa baada ya barua ya majibu kutoka Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Michezo (CAS] kuhusu kesi hiyo ya CAS 2025/A/11298 ambapo CAS imewarudisha kwenye mamlaka za michezo za ndani ya nchi.
“CAS imeielekeza Young Africans Sports Club kurudi kwanza kwenye Kamati za ndani za Soka ili kushughulikia kesi yetu kabla ya kurudi kwao kwa ajili ya hatua za rufaa.
“Lakini kutokana na uonevu, uvunjwaji mkubwa wa kanuni na upendeleo wa dhahiri kwa baadhi ya timu unaoendelea kufanywa na Mamlaka za soka Tanzania, Uongozi wa Young Africans Sports Club hauna imani na hauko tayari kupeleka shauri hilo kwenye Mamlaka ambazo zinatenda dhulma,” imeelezwa kwenye taarifa ya Yanga.
Aidha, Uongozi wa Yanga umefafanua kuwa Wanayanga wote, watakuwa tayari kuipambania haki yao kivyovyote vile ili kukomesha dhulma na uvunjwaji mkubwa wa kikanuni unaoendelea kufanywa na Mamlaka za soka kwa maslahi mapana ya maendeleo ya soka nchini.
Got a Questions?
Find us on Socials or Contact us and we’ll get back to you as soon as possible.