Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu amethibitisha kutokea kwa vifo vya Watu watatu ambao wamefariki dunia katika Kata ya Mbokomu, Wilaya ya Moshi, mkoani Kilimanjaro, baada ya kuangukiwa na ukuta wa nyumba yao kufuatia mvua kubwa zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali mkoani humo.
Mvua hizo pia zimesababisha athari mbalimbali ikiwemo uharibifu wa miundombinu na makazi.
RC Babu amewataka Wananchi kuendelea kuchukua tahadhari na kufuata maelekezo yanayotolewa na wataalamu na viongozi.
Taarifa zaidi Zitakujia, Endelea kufuatilia kurasa zetu kwenye Mitandao yakijamii @Wasafi FM
Mvua kubwa Moshi, Watu watatu wafariki dunia

Leave a Reply